Heka Heka Za Maisha | Iringo SDA Choir

Chief

Chief of Sinners.

Heka Heka Za Maisha - Iringo SDA Choir -Lyrics​

1.
Heka heka za Maisha, tumetingwa tumebanana
Mbio mbio asubuhi, kutwa nzima shughuli
Jioni tumechoka twalala hoi, Mungu hana nafasi tena kwetu
Udhuru ni mwingi sana, eti tunatafuta maisha
Yote ni ubatili na upepeo, mpe Mungu nafasi ya kwanza

(Wewe umetingwa umebanana, heka heka hauna muda
Maombi hushiriki, eti wafukuza Maisha
Sote tumetingwa shughuli, na masumbufu ya kila siku
Toa nafasi Mungu atawale, usikatae kazi ya bwana
Hekaheka za maisha na shughuli nyingi, zisifanye umwache Mungu
) x2

2.
Toa nafasi kwa Mungu, kwa ibada na matoleo
Usione ni hasara, Mungu kumuabudu
Usikatae kazi fungua moyo, tenga muda sema na Mungu wako
Upangapo mambo yako, Mungu na awe wa kwanza
Tafuta kwanza ufalme wa Mungu, mengine utapewa ziada

(Wewe umetingwa umebanana, heka heka hauna muda
Maombi hushiriki, eti wafukuza Maisha
Sote tumetingwa shughuli na masumbufu ya kila siku
Toa nafasi Mungu atawale, usikatae kazi ya bwana
Hekaheka za maisha na shughuli nyingi, zisifanye umwache Mungu
) x3
 
Back
Top